Sep 29, 2020 12:28 UTC
  • Maduro: Iran na Venezuela zina haki ya kuainisha mustakbali wao

Rais wa venezuela ameashiria vikwazo vya upande mmoja vya Marekani na kusisitiza kuwa nchi kama Iran na Venezuela zina haki ya kuainisha mustakbali wao katika suala la amani na uthabiti.

Rais Nicolas Maduro ameashiria hatua za Marekani za kujichukulia maamuzi ya upande mmoja dhidi ya Iran na Venezuela na kueleza kuwa wananchi walio huru na wanaojitegemea wanataka kukomeshwa mateso, jinai za uhalifu na mzingiro; masuala ambayo yanatishia maendeleo na ustawi wa wananchi.  

Akizungumzo katika kikao cha 75 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Rais wa Venezuela ameitaja Marekani kuwa tishio kuu kwa amani duniani. 

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela 

Rais Maduro ameyatamka hayo katika hali ambayo Marekani katika wiki za karibuni imemuwekea Rais huyo wa Venezuela vikwazo vipya kwa kwa sababu ya kile kilichotajwa kuwa kushirikiana na Iran. 

Marekani na baadhi ya waitifaki wa nchi hiyo katika miaka ya karibuni wameiwekea vikwazo serikali ya Venezuela kwa lengo la kuipindua ; njama ambayo hata hivyo imegonga mwamba. 

Tags

Maoni