Oct 19, 2020 15:27 UTC
  • Emmanuel Macron
    Emmanuel Macron

Serikali ya Ufaransa imekusudia kuwafukuza Waislamu wapatao 231 wanaoishi nchini humo kwa madai ya kujihusisha na vitendo vya kupindukia mpaka.

Uamuzi huo umechukuliwa siku mbili baada ya raia mmoja aliyetajwa kuwa na "misimamo mikali" kumuua mwalimu mmoja wa historia wa nchi hiyo.
Hadi sasa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Ufaransa haijatoa maelezo zaidi kuhusu mpango huo wa kuwafukuza mamia ya Waislamu nchini humo. 

Ijumaa iliyopita mwanafunzi aliyekuwa na asili ya Chechnia alimuua mwalimu wake baada ya kuwaonyesha wanafunzi darasani picha na vibonzo vinavyomdhalilisha na kumvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) kwa hoja eti ya uhuru wa kusema. Mwanafunzi huyo pia alipigwa risasi na kuuawa na polisi wa Ufaransa. 

Baada ya mauaji ya mwalimu huyo katika kiunga cha Paris siku ya Ijumaa iliyopita, serikali ya Rais Emmanue Macron wa Ufaransa imekuwa chini ya mashinikizo ya vyama na makundi ya mrengo wa kulia yanayotaka kuzidishwa ukandamizaji na mbinyo dhidi ya wahajiri. 

Ufaransa ambayo ndiyo nchi yenye idadi kubwa zaidi ya jamii ya Waislamu barani Ulaya, imekuwa ikishuhudia wimbi kubwa la hujuma na vitendo vya chuki na udhalilishaji dhidi ya Uislamu kwa lengo la kuharibu jina la dini hiyo na Mtume Muhammad (saw).

Mwezi uliopita wa Septemba Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa alitetea kitendo cha jarida la nchi hiyo la Charlie Hebdo cha kuchapisha tena vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad (saw) akisema kuwa ni 'uhuru wa kusema na kujieleza'. Hii ni licha ya kwamba, Ufaransa ni miongoni mwa nchi za Magharibi zilizopiga marufuku uhuru wa kutoa maoni, kuhoji au kudadisi madai ya kuuliwa Mayahudi milioni tatu katika Vita vya Pili vya Dunia. 

Tags