Oct 22, 2020 12:25 UTC
  • Trump arudia ndoto zake za kuzungumza na Iran

Rais wa Marekani, Donald Trump kwa mara nyingine amerudia ndoto yake ya kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran iwapo atashinda urais.

Akizungumza kwenye kampeni za uchaguzi katika mji wa Gastonia wa jimbo la Carolina Kaskazini, Trump amesema leo Alkhamisi kwa majira ya eneo hilo kwamba iwapo atachaguliwa kuwa rais wa Marekani katika uchaguzi wa tarehe 3 Novemba 2020, nchi ya kwanza atakayoipigia simu kufanya nayo mazungumzo na Iran.

Trump amekuwa akirudia mara kwa mara ndoto yake hiyo. Akiwa katika kampeni za uchaguzi katika jimbo la Nevad pia, rais huyo wa Marekani alimshutumu mpinzani wake wa chama cha Democrats, Joe Biden na kusema kuwa, nchi ya kwanza ambayo yeye Trump atazungumza nayo kwa simu mara baada ya kuchaguliwa kuwa rais wa Marekani, itakuwa ni Iran.

 

Trump na viongozi wengine wa ngazi za juu wa serikali yake akiwemo waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Mike Pompeo, mara kwa mara wamekuwa wakionesha hamu yao kubwa ya kufanya mazungumzo na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran lakini Tehran inakataa katakata.

Baada ya Trump na serikali yake kujitoa katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA hapo tarehe 8 Mei 2018 pamoja na kuwawekea wananchi wa Iran vikwazo vya kiwango cha juu mno kama wanavyojigamba wenyewe viongozi hao wa Marekani, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilitangaza wazi kuwa kamwe haitofanya mazungumzo na viongozi wa serikali ya Trump. 

Hatua hiyo ya Trump inaendelea kulaania vibaya ndani na nje ya Marekani huku Tehran ikisimama kwenye msimamo wake wa kukataa mazungumzo na serikali ya Trump, suala ambalo linaonekana ni pigo kubwa kwa rais huyo wa Marekani na serikali yake.

Tags

Maoni