Oct 23, 2020 11:00 UTC
  • Vladimir Putin
    Vladimir Putin

Rais wa Russia amesema kuwa udhibiti wa madola makubwa duniani umefikia kikomo na kwamba Moscow itajibu hatua yoyote ile ya kihasa na serikali ya Washington.

Rais Vladimir Putin wa Russia ametahadharisha kuhusu hatua yoyote ya kichokozi dhidi ya nchi hiyo na kusema: Russia itajibu uchokozi wa aina yoyote. 

Putin amesema kuwa, dunia imo katika hali ya mabadiliko, na kipindi cha udhibiti wa nchi kubwa kimeyoyoma; na nchi kama Marekani pia zitasombwa na mabadiliko hayo. 

Rais wa Russia amekosoa ushindani wa silaha duniani na kusema: Iwapo hakutawekwa mpaka wa ushindani huo dunia haitakuwa na mustakbali. 

Donald Trump na Vladimir Putin

Vilevile amashiria vita na mapigano ya sasa baina ya nchi za Armenia na Azerbaijan katika eneo la Nagorno-Karabakh na kusema: Rusia ina uhusiano na nchi hizo mbili na kile kinachojiri sasa katika eneo hilo ni maafa ambayo yanapaswa kukomeshwa. 

Mazungumzo ya kudhibiti silaha za maangamizi baina ya Marekani na Russia yamegonga mwamba katika miezi ya karibuni kutokana na vizingiti na ukwamishaji wa serikali ya Washington. Maafisa wa Russia pia wamepinga masharti yaliyotolewa na Marekani kwa ajili ya kurefusha mkataba wa kudhibiti silaha za nyuklia wa New START.  

Tags

Maoni