Oct 23, 2020 11:23 UTC
  • Trump kuziarifisha taasisi za kimataifa za kutetea haki za binadamu kuwa ni

Serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani ina nia ya kuziarifisha taasisi na jumuiya za kimataifa za kutetea haki za binadamu kuwa "zinapiga vita Uyahudi" (Antisemitism).

Gazeti la Politico la Marekani limeripoti kuwa, serikali ya Donald Trump imechukua uamuzi wa kuyatangaza mashirika kadhaa ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu ikiwemo Amnesty International, Human Rights Watch na Oxfam kuwa ni mashirika "yanayopiga vita Uyahudi" kutokana na kukosoa siasa za kihasa na za kibaguzi za Israel na uungaji mkono wa mashirika hayo kwa harakati ya kimataifa ya kususuia bidhaa za utawala huo haramu ya Boycott, Divestment and Sanctions (DBS). 

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, Mike Pompeo pia ameunga mkono mpango wa kuyaarifisha mashirika hayo ya kutetea haki za binadamu kuwa ni dhidi ya Uyahudi.

Ripoti ya gazeti la Politico imesema Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Marekani, siku kadhaa zijazo atatoa taarifa ya kuyatangaza mashirika hayo kuwa ni "dhidi ya Uyahudi" na kukata misaada ya Marekani kwa mashirika hayo ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu.

Askari wa Israel wakimnyanyasa mtoto wa Kipalestina

Gazeti la Politico limeandika kuwa: Lengo la hatua hiyo ya serikali ya Trump ni kupata kura za wapigaji kura wanaoiunga mkono Israel.

Marekani ndiyo mtetezi na mfadhili mkubwa zaidi wa utawala haramu wa Israel unaoendelea kuua raia wasio na hatia wa Palestina na kupora ardhi zaidi za taifa hilo.  

Tags