Oct 25, 2020 07:57 UTC
  • Mhadhiri mkongwe wa Marekani atabiri kushindwa Trump katika uchaguzi wa rais

Mhadhiri mkongwe wa vyuo vikuu nchini Marekani ametabiri kuwa rais wa sasa wa nchi hiyo atashindwa katika uchaguzi ujao wa rais; na kwa msingi huo atakuwa ameongoza kwa kipindi kimoja tu.

Profesa Allan Lichtman ambaye ametoa utabiri sahihi katika utabiri wake wote kuhusu matokeo ya uchaguzi nchini Marekani tangu mwaka 1984, ameeleza kuwa: Donald Trump atakuwa rais wa kwanza kushindwa uchaguzi wa katika muhula wa pili baada ya George Bush baba tangu mwaka 1992. 

Profesa Allan Lichtman atabiri kushindwa Trump katika uchaguzi ujao 

Aghalabu ya chunguzi za maoni zilizofanywa nchini Marekani zinaonyesha kuwa Joe Biden mgombea wa chama cha Democratic anaongoza katika kinyang'anyiro cha uchaguzi uliopangwa kufanyika Novemba 3 mwaka huu. 

Uchunguzi wa maoni uliofanywa siku chache zilizopita na gazeti la New York Times unaonyesha kuwa asilimia 50 ya watu walioshiriki katika uchunguzi huo wanamuunga mkono Biden na asilimia 41 wanamuunga mkono Trump.  

Katika upande mwingine, zaidi ya asilimia 52 ya watu walioshiriki katika uchunguzi wa maoni wa CNN ambao ulifanywa mara baada ya mdahalo wa mwisho wa wagombea hao wawili wa kiti cha rais nchini Marekani wamesema kuwa Biden ndiye mshindi wa mdahalo huo na asilimia 39 walitoa maoni yao kuhusu Trump. 

Tags

Maoni