Oct 28, 2020 04:21 UTC
  • Hotuba ya Zarif kwa mnasaba wa miaka 75 ya kuasisiwa UN; kubainisha wasiwasi na matumaini

Umoja wa Mataifa uliasisiwa miaka 75 iliyopita ukiwa na malengo mawili. Mosi kulinda na kuimarisha amani duniani.

Pili, kuandaa uwanja na mazingira ya kuongeza ushirikiano kadiri inavyowezekana baina ya mataifa ya dunia katika uga wa mahusiano ya kimataifa. Hata hivyo mpaka leo kungali kuna swali la kimsingi nalo ni kuwa, je taasisi hii kubwa kabisa imekuwa na utendaji mzuri na unaofaa katika kipindi chote hiki cha historia yake?

Akihutubia Jumatatu ya juzi kwa manasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 75 tangu kuasisiwa Umoja wa Mataifa, Dakta Muhammad Javad Zarif, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Iran alitoa majibu ya swali hili wakati alipodadisi mchango wa umoja huo katika kurejesha amani na usalama wa kimataifa baada ya vita viwili vya kutisha vya kwanza na vya pili vya dunia. Dakta Zarif alisema: Kwa mujibu wa utafiti mpya uliofanyika, kuanzia mwaka 2001 ambao ulijulikana kama 'Mwaka wa Mazungumzo Baina ya Tamaduni Mbalimbali' watu milioni 27 wamelazimika kuwa wakimbizi ikiwa ni matokeo ya 'vita vya daima' vya Marekani.

 

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameashiria pia vita vinane vya utumiaji mabavu vya Marekani ambapo kuanzia mwaka 2001 Washington ilianzisha vita hivyo au ilijiunga navyo chini ya anuani ya 'vita dhidi ya ugaidi' na kubainisha ukweli mchungu ambao ni kwamba, vita hivi vimepelekea mamia ya maelfu ya roho za watu wasio na hatia zipotee bure bilashi, huku idadi kubwa ya wanajamii na familia zikilazimika kutangatanga.

Matamshi ya Dakta Zarif katika uwanja huu, yanaashiria nukta mbili muhimu katika kushindwa Umoja wa Mataifa kuwa na nafasi athirifu na ya utendaji unaofaa zaidi:

Nukta ya kwanza; mapungufu ambayo yaliugubika muundo wa Umoja wa Mataifa tangu awali. Masuala kama kura ya veto na kuhodhi mambo baadhi ya wanachama tu ni mambo ambayo yamekuwa na mchango katika mapungufu haya.

Murad-enadi mtaaamu wa masuala ya kimataifa anasema kuwa, moja ya kigugumizi kikuu cha Umoja wa Mataifa kinapatikana katika kipengee cha cha faslu ya tano ya umoja huo ambacho kinahusiana na Baraza la Usalama hususan kipengee cha 27 ambacho kinawapa haki ya veto wanachama watano wa kudumu wa baraza hilo. Mtaalamu huyo anasema: Jambo hili limepelekea kupatiwa mamlaka maalumu wanachama wa kudumu wa Baraza la Usalama ambao wamekuwa wakitumia fursa hiyo kuzuia na kukwamisha mafanikio ya Umoja wa Mataifa.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa

 

Nukta ya pili; kutangulizwa matashi ya kisiasa kwenye nguzo muhimu za umoja huo na kuwa na taathira mashinikizo na uingiliaji ulio nje ya ustahiki wa Marekani kwa asasi hiyo ambapo kutokana na kigugumizi cha jamii ya kimataifa, ubabe huo wa Washington umekuwa ukiongezeka siku baada ya siku.

Kukaliwa kwa mabavu Afghanistan na baada ya hapo kushambuliwa Iraq mwaka 2003 kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi na silaha za maangamizi ya umati, yalikuwa mambo mawili ya uzushi na uongo mkubwa wa Marekani, ambayo hayakuwa na himaya yoyote ile ya kisheria katika sheria za kimataifa. Kuanzisha Marekani vita hivyo bila ya idhini ya kisheria, kimsingi ilikuwa ni kuuzunguka Umoja wa Mataifa.

Kadhia ya leo pia ni kuwa, kuibuka mambo mapya kama kushadidi misimamo ya uchukuaji maamuzi ya upande mmoja na kutumia vibaya wenzo wa vikwazo katika uga wa mfumo wa kimataifa ni mambo ambayo yameufanya Umoja wa Mataifa ukabiliwe na changamoto kubwa katika kwenda sambamba na mazingira ya sasa.

Kura ya veto

 

Katikka kubainisha maana ya ndani zaidi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema bayana kwamba: Vipi itawezekana kuizuia nguvu ambayo imeshiriki katika matukio 220 ya vita kati ya matukio 244 ya vita katika historia yake, kuanzia vita dhidi ya watu wa asili wan chi yake, vita dhidi ya jamii ya watumwa ambao waliuawa kinyama na kikatili mpaka katika vita 39 vya kijeshi na takribani vita 120 vya kiuchumi kuanzia mwaka 1945.

Ni kwa kuzingatia hali hii na ushahidi huu ndipo Dakta Zarif akakumbusha kwa kusema kwamba, wakati wa kufanyika mageuzi uko wazi. Na kimsingi hiki kimekuwa kilio cha muda mrefu cha mataifa mengi ya dunia ambayo yanataka kuweko mabadiliko katika muundo wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Tags