Oct 29, 2020 12:17 UTC
  • Denmark yaunga mkono hatua za Ufaransa za chuki dhidi ya Uislamu

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Denmark ametangaza kuunga mkono hatua za serikali ya Ufaransa zilizo dhidi ya Uislamu na ambazo zimezusha malalamiko na maandamano katika maeneo mbalimbali ya ulimwengu wa Kiislamu.

Akizungumza katika mahojiano aliyofanyiwa Jeppe Kofod, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Denmark ameunga mkono madai ya Rais wa Ufaransa kwamba, hatua ya gazeti la Charlie Hebdo ya kuchapisha vibonzo na vikatuni vinavyomvunjia heshima Bwana Mtume SAW ni katika uhuru wa kutoa maoni.

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Denmark amedai kuwa, uhuru wa kujieleza ni thamani muhimu na ya kimsingi katika demokrasia na kwamba, nchi yake inatangaza kuwa pamoja na serikali ya Ufaransa katika kadhia hiyo.

Matamshi hayo ya kifidhuli ya Jeppe Kofod anayatoa katika hali ambayo, hatua ya Ufaransa ya kumvunjia heshima Bwana Mtume SAW imeendelea kulalamikiwa na kulaaniwa kila kona ya ulimwengu wa Kiislamu.

Maandamano ya kulaani matamshi ya chuki dhidi ya Uislamu ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa

 

Madai ya uhuru wa kujieleza yanatolewa katika hali ambayo, walimwengu wanahoji kwa anayeandika kuhusu kutiliwa shaka mauaji yaHolocaust anafungwa jela, lakini kumtusi Mtume Mtukufu SAW kunaruhusiwa?

Hatua ya Rais Emmanuel Macron ya kutoa matamshi ya jeuri dhidi ya Uislamu na kutangaza kuwa, Ufaransa itaendelea kusambaza katuni na vibonzo vinavyomdhalilisha Mtume Muhammad (SAW), imeughadhabisha mno Umma wa Kiislamu.

Maandamano ya kulaani kitendo hicho yameshuhudiwa katika nchi kadhaa za Kiislamu na Kiarabu kama vile Iran, Pakistan, Iraq na Bangladesh, huku mwito wa kususiwa bidhaa za Ufaransa katika nchi hizo ukishika kasi.

Maoni