Oct 30, 2020 02:46 UTC
  • Trump akiri: Hakuna uhuru wa vyombo vya habari nchini Marekani

Tangu aliposhika madaraka ya nchi Januari mwaka 2017, Rais Donald Trump wa Marekani daima amekuwa akihujumu vikali vyombo vya habari vinavyomkosoa yeye na utendaji wa serikali yake.

Japokuwa ukosoaji huo kwa sehemu kubwa ulitokana na vyombo hivyo kutokwenda sambamba na mieleleo na sera zake, lakini jambo hilo pia linaakisi uhakika usiokanushika, yaani kutokuwepo uhuru wa vyombo vya habari nchini Marekani. 

Katika msimamo wake wa karibuni kwenye uwanja huo,Trump ameandika katika mtandao wa Twitter kwamba, vyombo vya habari vya Marekani ni vya kifisadi na amekosoa kutokuwepo uhuru wa vyombo hivyo nchini humo.Trump ameandika kuwa: "Marekani haina uhuru wa vyombo vya habari. Tunakandamiza taarifa au tuna habari feki na bandia. Katika kipindi cha wiki mbili zilizopita imebainika ni kwa kiwango gani vyombo vyetu vya habari vilivyo vya kifisadi, na sasa inabainika kuwa hata makampuni makubwa ya teknolojia ni mabaya zaidi."

Image Caption

Katika hotuba na jumbe zake nyingi kwenye mitandao ya kijamii hususan katika miezi na siku hizi za kuelekea kwenye uchaguzi wa rais, Donald Trump amekuwa akivishambulia vyombo vya habari na kuzitaja habari za vyombo hivyo kuwa ni bandia na za uongo. Trump, kama kiongozi wa nchi inayodai kuwa kinara wa uhuru duniani, anaamini uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza ambao unamsifia, "kumtukuza" na kusifu utendaji wake, na kamwe hawezi kuvumilia ukosoaji wa aina yoyote wa kazi au siasa zake. Mtandao wa kijamii wa Twitter umekuwa ukitaja jumbe za Trump kuwa ni kielelezo cha upotoshaji na kuzifungia. Kwa mfano tu wiki mbili zilizopita Twitter ilifunga ukurasa wa timu ya kampeni za uchaguzi wa rais ya Trump baada ya kutangaza kuwa, kampeni zake zinazomtangaza mpinzani wake mkuu katika uchaguzi ujao, Joe Biden kuwa ni "kidhabi", zimekiuka sera za chombo hivyo.       

Pamoja na hayo tunapotupia jicho utendaji wa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii nchini Marekani tunakutala na kitu kinachoitwa udhibiti wa kundi dogo la watu mafisadi wa vyombo vya habari (Media oligarchy). Kwa maneno mengine ni kuwa, makampuni makubwa yanayomiliki vyombo vya habari kama magazeti, kanali za televisheni, redio na televisheni za satalaiti na makampuni makubwa ya teknolojia kama Google, Microsoft, Facebook, Twitter na Instagram yanafanya kazi kwa maslahi ya Marekani. Mara nyingi makampuni na mashirika haya hurusha hewani au kutangaza habari na ripoti zinazooana na mitazamo makhsusi na sera maalumu, na hata habari za kawaida za makampuni, vyombo vya habari na mitandao hiyo ya kijamii kuhusiana na matukio mbalimbali huchujwa, kupotoshwa au kuchambuliwa kwa njia maalumu na kwa malengo na mwelekeo makhsusi. Mashirika na makampuni hayo hufutilia mbali au kuficha habari na ripoti zinazokwenda kinyume na siasa zinazolinda maslahi ya serikali ya Marekani au makundi ya mabepari na wamiliki wake.  

Hali hii inashuhudiwa zaidi katika mitandao ya kijamii na imeitia wasiwasi hata Kongresi ya Marekani yenyewe. Ripoti yenye kurasa 449 ya Kongresi ya Marekani iliyochunguza sera za ushindani za mashirika makubwa ya teknolojia kwa kipindi cha miezi 16 imetangaza kuwa, makampuni ya Apple, Amazon, Facebook na Google yanatumia sera za ukiritimba (Monopolistic Policies). Wakati huo huo Twitter, Instagram na Facebook kama mitandao ya kijamii ya Kimarekani yenye watumiaji wengi duniani, imekuwa ikifunga kurasa za watu, maafisa wa serikali na taasisi za nchi mbalimbali hususan nchi wapinzani wa siasa za Marekani kama Ruusia, China, Iran na Venezuela. Makampuni hayo ya mitandao ya kijamii yanachukua hatua kama hizo ili kwa madai yao kuzuia upashaji habari unaokwenda kinyume na maslahi ya serikali ya Washington. Hii ni licha ya kwamba katika zama za sasa ambazo ni zama za mapinduzi ya mawasiliano, ni vigumu sana na pengine muhali kuzuia pashaji habari kutokana na wingi na aina mbalimbali za vyombo vya upashaji habai kuanzia mtandao wa intaneti, satalaiti, redio, televisheni na kadhalika.    

Tags

Maoni