Oct 31, 2020 11:04 UTC
  • Bernie Sanders
    Bernie Sanders

Seneta wa jimbo la Vermont na mwanasiasa mashuhuri wa Marekani, Bernie Sanders amemtaja Rais Donald Trump wa nchi hiyo kuwa ni kidhabi, na kusisitiza kuwa uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika tarehe 3 Novemba mwaka huu nchini humo ndio muhimu zaidi katika historia ya Marekani.

Bernie Sanders amesema Donald Trump amepatwa na maradhi ya kusema uongo na kwa kwamba uchaguzi wa rais wa Novemba 3 ndio muhimu zaidi katika kipindi chote cha maisha ya Wamarekani. 

Sanders ameongeza kuwa, Wamarekani hawawezi kuwa na serikali isiyoamini elimu na sayansi. Vilevile amemkosoa Donald Trump kwa kufanya jitihada za kudhoofisha demokrasia nchini Marekani. 

Seneta huyo wa jimbo la Vermont amemtaja Trump kuwa ni mtu mwenye fikra za kidikteta anayefanya jitihada za kudhoofisha demokrasia.

Trump na Sanders

Katika kampeni zake za uchaguzi wa rais, Donald Trump amekuwa akitangaza dhana yake ya kufanyika udanganyifu katika uchaguzi ujao wa rais nchini Marekani.

Uchunguzi mwingi wa maoni unaonyesha kuwa, mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democratic, Joe Biden, anaongoza akimuacha nyuma Donald Trump anayewakilisha chama cha Republican.

Siasa zenye migongano, maamuzi na mienendo ya kustaajabisha, uongozi mbaya na uzembe na kufeli kukabiliana na maambukizi ya virusi vya corona vilivyosababisha vifo vya zaidi ya Wamarekani laki mbili na 35 elfu, yote hayo yameshusha chini umaarufu wa kiongozi huyo baina ya Wamarekani.     

Tags

Maoni