Oct 31, 2020 11:05 UTC
  • Justin Trudeau
    Justin Trudeau

Waziri Mkuu wa Canada amejitenga tena na mienendo ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ya kuhalalisha na kutetea matusi na kuvunjiwa heshima itikadi na matukufu ya Uislamu kwa kisingizio cha "uhuru wa kusema na kujieleza" na kusisitiza kwamba, uhuru huo una mipaka yake.

Justin Trudeau ametetea uhuru wa kusema na kujieleza lakini amesisitiza kuwa si jambo mutlaki na lisilo na mpaka, na kwamba uhuru huo haupasi kutumiwa kwa ajili ya kuudhi sehemu ya jamii. 

Trudeau amesema kuwa Canada italinda uhuru wa kusema lakini uhuru wa kusema wenye mipaka.

Waziri Mkuu wa Canada amesema kuwa ni wajibu kuheshimu itikadi za watu wengine na kujiepusha kuwaudhi watu tunaoshirikiana nao masuala ya kijamii na maisha. Amesisitiza kuwa uhuru wa kusema na kujieleza unapaswa kutumiwa kwa hadhari. 

Amesisitiza kuwa: "Katika jamii yenye matabaka ya watu wenye tamaduni na itikadi tofauti na inayofuata misingi ya kuheshimiana, ni muhimu kuwa macho kuhusiana na matamshi na matendo yetu kuhusiana na matabaka ya watu wengine hususan jamii za wananchi wanaoendelea kubaguliwa." 

Katika matamshi yake ya awali, Waziri Mkuu wa Canada, Justin Trudeau alikuwa amesema kuwa gaidi aliyetekeleza hujuma ya kigaidi katika mji wa Nice nchini Ufaransa hawakilishi dini ya Uislamu wala Waislamu, na kwamba watu wote wanapasa kukiri ukweli huo.
Hata hivyo Justin Trudeau amesisitiza kuwa, watu wa aina hii hawawakilishi dini ya Uislamu. isla

Matamshi haya ya Waziri Mkuu wa Canada yanatofautiana na yale yaliyotolewa na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa na serikali yake ambao wanang'ng'ana kuuhusisha ugaidi na dini ya Uislamu.

Rais huyo wa Ufaransa aliunga mkono jinai ya mwalimu mmoja wa Ufaransa ya kuwaonesha wanafunzi vibonzo vinavyomvunjia heshima Mtume Muhammad SAW kiasi kwamba hata alimpa nishani ya ushujaa mwalimu huyo baada ya kuuliwa na mtu mmoja mwenye hasira.

Nchi za Kiislamu zimelaani vikali uchochezi huo wa rais wa Ufaransa. Maandamano makubwa yanaendelea kufanyika katika ulimwengu wa Kiislamu kulaani uchochezi huo wa Emmanuel Macron.

Maoni