Nov 16, 2020 02:34 UTC
  • CNN: Donald Trump ni sawa na Adolf Hitler

Televisheni ya CNN ya Marekani imeripoti kuwa, hatua na mienendo ya rais wa sasa wa nchi hiyo, Donald Trump katika kipindi cha miaka minne iliyopita inafanana na ya watawala wa zamani wa Ujerumani ya Manazi.

Mwandishi wa CNN Christiane Amanpour amesema kuwa hatua zilizochukuliwa na Rais Donald Trump katika kipindi cha uongozi wake wa miaka minne zinafanana na za dikteta wa zamani wa Ujerumani, Adolf Hitler na viongzo wa utawala wa manazi wa nchi hiyo katika kipindi cha Vita vya Pili vya Dunia. 

Mwandishi huyo wa CNN amesema kuwa, Doland Trump anafanya operesheni ya kusafisha na kuwafutilia mbali wale wote anaodai kuwa ni maadui zake.

Christiane Amanpour ameongeza kuwa, Trump anakwamisha na kuzuia mchakato wa kukabidhiana madaraka kwa amani baada ya uchaguzi wa rais wa tarehe 3 mwezi huu wa Novemba nchini Marekani. 

Trump angali anasisitiza kuwa, anamini ataibuka mshindi katika kinyang'anyiro hicho licha ya taarifa za awali kuonesha kuwa, mpinzani wake wa chama cha Democratic, Joe Biden ameshinda kwa kupata kura nyingi za wananchi na za wajumbe wa Electoral College. 

Wanamgambo wafusi wa Trump

Juzi Jumamosi waungaji mkono wa Trump walifanya maandamano mjini Washington wakiongozwa na baadhi ya makundi yenye misimamo mikali ya mrengo wa kulia kama lile linalojiita Proud Boys. Maandamanao hayo yalishuhudia ghasia na mapigano baina ya wafuasi wa Trump na wapinzani wake walioongozwa na kundi la Anti-fascism, (ANTIFA).

Tags