Nov 19, 2020 12:04 UTC
  • Madai ya Bolton kuhusu juhudi zinazofanywa na Trump kufikia mapatano na Iran

Mashauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Marekani, bila ya kuashiria siasa za uadui wa nchi hiyo dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amedai kwamba Rais Donald Trump wa nchi hiyo anataka kufanya mazungumzo na Iran.

Huku akikariri madai yasiyo na msingi ya viongozi wa White House dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, John Bolton amesema kuwa Trump hatakubali matokeo ya uchaguzi uliofanyika hivi karibuni huko Marekani na kwamba katika siku chache zijazo ataanzisha juhudi za kukutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Iran.

Bolton ametupilia mbali ripoti iliyochapishwa karibuni na gazeti la New York Times iliyosema kuwa Trump amekuwa na mipango ya kuishambulia kijeshi Iran na kuongeza kuwa kama kuna ukweli wowote katika madai hayo, basi suala hilo litakuwa limetokana na mbinu za kuchanganyikiwa, zisizo za kawaida, za kipumbavu na zisizozingatia ukweli wa mambo.

Moja ya manowari za Iran

Trump na viongozi wengine wa White House wamekuwa wakizungumzia mara kwa mara madai ya kutaka kufanya mazungumzo na Iran. Hii ni katika hali ambayo viongozi wa Iran wamesisitiza mara si moja kwamba njia pekee ya kufanyika mazungumzo kama hayo ni kwa Marekani kurejea katika mapatano ya kimataifa ya JCPOA.

Gazeti la New York Time liliandika Jumatatu kwamba katika kikao chake na maafisa wa ngazi za juu wa kijeshi na kidiplomasia wa Marekani, Trump alitoa pendekezo la kushambulia vituo vya nyuklia vya Iran jambo lililopingwa vikali na maafisa walioshiriki kikao hicho.

Kufuati uvumi huo, Alireza, Mir Yusefi, Msemaji wa Ofisi ya Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika Umoja wa Mataifa alisema kuwa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ina uwezo wa kutumia nguvu zake kubwa za kijeshi katika kujitetea au kuzuia chokochoko zozote za adui dhidi yake.

Tags