Nov 22, 2020 12:28 UTC
  • Wamarekani wapatao milioni 100 wanakabiliwa na hatari ya kukumbwa na baa la njaa

Ripoti za taasisi za serikali ya Marekani zinaonyesha kuwa maambukizi ya virusi vya corona yamewafanya raia wapatao milioni 100 wa nchi hiyo wakabiliwe na hatari ya kukumbwa na baa la njaa.

Kanali ya televisheni ya MSNBC imeripoti kuwa, taasisi za serikali nchini Marekani zimetahadharisha kuwa, kutokana na athari za mripuko wa virusi vya corona, watu wapatao milioni mia moja hawajui katika siku zijazo vipi na wapi wataweza kupata chakula cha kujikimu.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kuna mamilioni ya watu nchini Marekani ambao wanaishi wakiwa hawana uhakika wa kupata chakula.

Imeelezwa kuwa kumalizika muhula wa mpango wa msaada wa serikali, ukiwemo wa dola 600 zilizokuwa zikitolewa kila wiki na serikali kuu ya Marekani ili kuwasaidia wananchi katika kipindi cha corona, yumkini kumechangia kuongezeka kwa umasikini nchini humo.

Katika siku za karibuni, vyombo vya habari vimeonyesha taswira za misururu mirefu ya magari yaliyopanga foleni kwa ajili ya kupokea msaada wa chakula cha bure katika majimbo mbalimbali ya Marekani likiwemo la Texas.

Ripoti hizo zinatolewa huku kukiendelea kushuhudiwa mvutano kati ya bunge la Marekani la Kongresi na serikali ya nchi hiyo juu ya upitishaji wa bajeti mpya ya fedha za msaada.../

Tags