Nov 24, 2020 02:23 UTC
  • Ufaransa yashiriki kwa kiwango kikubwa kuangamiza raia nchini Yemen

Vyombo vya habari vya Ufaransa vimefichua kuwa, serikali ya nchi hiyo inashiriki vilivyo katika kutoa mafunzo kwa wanajeshi wa Saudi Arabia na kuwaua kwa umati wananchi wa Yemen.

Mkoloni mkongwe wa Ulaya yaani Ufaransa, ana historia kubwa ya ukatili na mauaji ya watu wasio na hatia hasa katika nchi ya Kiafrika ya Algeria.

Televisheni ya al Masira ya Yemen imefichua matokeo ya uchunguzi uliofanywa na vyombo vya habari vya Ufaransa ambayo yamesema kuwa, mashirika ya Ufaransa yamekuwa yakishirikiana na ukoo wa Aal Saud kufanya ukatili na mauaji makubwa ya raia nchini Yemen tangu Saudi Arabia na kundi lake walipoivamia nchi hiyo maskini ya Kiarabu.

Emmanuel Macron, rais wa Ufaransa aliyeshindwa kuficha chuki zake dhidi ya Waislamu. Wanajeshi wa Macron wanashiriki kikamilifu kuua Waislamu wasio na hatia nchini Yemen

 

Kwa mujibu wa shirika la habari la Tasnim, Ufaransa muda wote huu wa uvamizi wa Yemen, imekuwa ikitoa mafunzo ya kijeshi kwa wanajeshi vamizi wa Yemen hasa mafunzo ya kutumia mizinga ambayo Ufaransa imeipa Saudi Arabia ili ifanye mauaji katika nchi ya Waislamu ya Yemen.

Vyombo vya habari vya UIngereza pia vimefichua kuwa, mashirika ya nchi hiyo yanashiriki kwa kiwango kikubwa katika kuongoza na kusimamia mashambulio ya anga pamoja na kuandaa ndege za kivita zinazotumika kufanya mauaji ya umati nchini Yemen.

Ripoti kuhusu kushiriki kikamilifu Marekani katika mauaji ya raia huko Yemen pia ziko nyingi na zimekuwa zikitangazwa mara kwa mara. Utawala wa Kizayuni wa Israel nao unashiriki bega kwa bega na wavamizi wa Yemen ambao kijuujuuu inaonekana kama vile wanaongozwa na Saudi Arabia.

Tags