Nov 27, 2020 02:29 UTC
  • Serikali ya Trump yazidi kutoa vitisho kuhusu uwezekano wa Marekani kurejea katika JCPOA

Mshauri wa Usalama wa Taifa wa serikali ya Donald Trump huko White House ameendelea kutoa vitisho alivyodai ni vya hatari ya Marekani kurejea katika mapatano ya kimataifa ya JCPOA.

Televisheni ya Bloomberg imemnukuu Robert O'Brien akionesha woga wake wa uwezekano wa kurejea Marekani katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA na kutoa vitisho kwa kudai kwamba kuilegezea kamba Iran kwa kiwango chochote kile kutaharatisha mchakato wa nchi za Kiarabu wa kutangaza uhusiano wao na utawala wa Kizayuni wa Israel.

Aidha amedai kwamba nchi za Kiarabu zilizotangaza uhusiano wa kawaida na Israel zimefanya hivyo kwa kuwa haziiamini Iran. Ametoa madai hayo katika hali ambayo hatua ya watawala vibaraka wa Imarati, Bahrain na Sudan ya kujidhalilisha mbele ya Wazayuni kwa kutangaza uhusiano wao wa kawaida na Israel inaendelea kulaaniwa katika ulimwengu mzima wa Kiarabu na Kiislamu.

Rais wa Maraekani, Donald Trump

 

Wananchi wa nchi za Kiarabu na Kiislamu wanaamini kwamba, watawala wa nchi hizo wameamua kutangaza uhusiano wa kawaida na utawala wa Kizayuni kutokana na kutokuwa na uthubutu wa kukataa amri za Marekani, kutokuwa na uungaji mkono wa wananchi wao na dhati ya watawala hao ya kuwa tayari kulinda tawala zao kwa gharama yoyote ile.

Nchi zilizotangaza uhusiano wa kawaida na Israel, hasa viongozi wa serikali ya mpito ya Sudan hawaonekani kujiamini hata kiadogo kiasi kwamba, mara kwa mara wanatoa matamshi ya kujaribu kupoza hasira za wananchi kufuatia serikali hiyo ya mpito kujidhalilisha kwa Wazayuni.

Tags