Nov 27, 2020 02:44 UTC
  • Foreign Policy: Iran ni imara zaidi ya walivyofikiria Marekani na Israel

Gazeti moja la Marekani limetangaza kuwa, White House na utawala wa Kizayuni wa Israel walikosea katika mahesabu yao kuhusiana na Iran kwani Tehran ni imara zaidi ya walivyodhani viongozi wa Marekani katika siasa zao za kuliweketa taifa la Iran vikwazo vya kiwango cha juu kupindukia.

Katika makala yake ya uchambuzi wa kina, gazeti la Foreign Policy la Marekani limeandika kuwa, siasa za serikali ya Donald Trump za kuiwekea Iran vikwazo vya kiwango cha juu kabisa vimeshindwa kuishawishi Tehran kufanya mazungumzo mapya kuhusu mapatano ya nyuklia ya JCPOA.

Itakumbukwa kuwa baada ya Marekani kujitoa kijeuri katika mapatano ya kimataifa ya nyuklia ya JCPOA tarehe 8 Mei, 2018, iliirejeshea Iran vikwazo vyote vilivyokuwa vimeondolewa baada ya kufikiwa mapatano hayo na iliiwekea Tehran mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa huku viongozi wa White House wakijigamba kwamba, hakuna nchi yoyote iliyowahi kuwekewa vikwazo vya kiwango cha juu kama hicho.

Wananchi wa Iran wamesambaratisha vikwazo vya Marekani kwa muqawama wao wa kiwango cha juu

 

Trump alidai kuwa, kwa kujitoa katika makubaliano ya JCPOA na kuiwekea Iran vikwazo vya kiwango cha juu kabisa, kutailazimisha Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kukubali kuburuzwa kwenye meza ya mazungumzo na kufikia mapatano mapya yanayotakiwa na Trump, bila ya hiari yake.

Sasa hivi miaka miwili imepita tangu Trump atoe majigambo hayo lakini yameendelea kuwa ndoto ya alinacha isiyoaguka

Muqawama wa kiwango cha juu uliooneshwa na Tehran mbele ya vikwazo vya kiwango cha juu vya Marekani umethibitisha kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kamwe haiwezi kufanya mazungumzo chini ya mashinikizo na vitisho, wala na nchi kama Marekani ambayo haina mwamana na haiheshimu hata ahadi zake inazozitoa mbele ya walimwengu wote.

Tags