Nov 28, 2020 04:37 UTC
  • Biden kuajiri wahudumu wa afya laki moja kufuatilia watu wenye maambukizi ya corona

Vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti kuwa, Joe Biden ana mpango katika serikali yake ijayo nchini humo kuajiri wahudumu wa afya wapya laki moja kwa lengo la kuwafuatilia wale wote wenye maambukizi ya virusi vya corona.

Joe Biden Rais mteule wa Marekani katika serikali yake mpya ana mpango wa kuajiri wahudumu wa afya laki moja ambao watafanya kazi ya kuwafuatilia watu wote wenye maambukizi ya corona ncini humo hata hivyo kuna uwezekano mpango wake huo ukapingwa na kongresi ya nchi hiyo. 

Mpango huo wa Biden kwa ajili ya kuwafuatilia waathirika wa corona utagharimu karibu dola bilioni 3.6. Mpango huo unatajwa huku Bunge la Wawakilishi la Marekani likikwama kuidhinisha bajeti ya kusaidia mapambano dhidi ya corona nchini humo; na Seneti ya nchi hiyo inayodhibiiwa na Warepublican ikipinga pia serikali ya federali kuongezewa jukumu la kushughulikia janga hilo la corona.  

Baadhi ya maafisa wa afya wa Marekani wamemuomba Biden atoe ajira ya kudumu kwa wahudumu hao wa afya ili waweze kutumika tena iwapo kutaibuka magonjwa mengine mapya nchini humo.   

Marekani hadi sasa inaongoza kwa kuwa na watu wengi wenye maambukizi ya corona duniani; na pia kwa kuwa na idadi kubwa ya watu walioaga dunia kwa ugonjwa wa Covid-19. 

Marekani inaongoza kwa kesi nyingi za corona 

 

Tags