Nov 28, 2020 07:46 UTC
  • Trump athibitisha kuhusika Mossad katika mauaji ya shahidi Fakhrizadeh

Hatua ya rais wa Marekani ya kuusambaza ujumbe ulioandikwa na mwandishi mmoja wa habari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel imethibitisha kwa njia isiyo ya moja kwa moja kuhusika utawala huo katika mauaji ya mwanasayansi wa nyuklia wa Iran.

Magaidi wenye silaha jana jioni waliishambulia gari iliyokuwa imembeba Mohsen Fakhrizadeh, Mkuu wa Shirika la Utafiti na Ubunifu la Wizara ya Ulinzi ya Iran na kumuua shahidi mwanasayansi huyo.

Kufuatia jinai hiyo ya kinyama, Rais Donald Trump wa Marekani ameamua kuutuma tena katika ukurasa wake wa Twitter ujumbe ulioandikwa na mwandishi wa habari wa Israel, ambaye amesema katika ujumbe wake huo kwamba shahidi Fakhrizadeh alikuwa akifuatiliwa kwa miaka kadhaa na shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni Mossad.

Ujumbe uliosambazwa tena na Trump

Wakati huo huo Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Mohammad Javad Zarif amelaani vikali hujuma hiyo ya kigaidi na kuongeza kuwa, kuna ushahidi mkubwa unaoonyesha kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel umehusika katika mauaji ya Fakhrizadeh, ambaye pia alikuwa profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Imam Hussein mjini Tehran.

Zarif amesisitiza kuwa Iran inaitaka jamii ya kimataifa na hasa Umoja wa Ulaya uache kutumia vigezo vya kuaibisha vya undumakuwili na kulaani kitendo hicho cha kigaidi.../

Tags