Dec 02, 2020 07:01 UTC
  • Trump amejikusanyia dola milioni 170 kwa kudai udanganyifu katika uchaguzi wa Marekani

Vyombo vya habari vya Magharibi vimetangaza kuwa, rais wa Marekani, Donald Trump hadi sasa ameshajikusanyia ziadi ya dola milioni 170 kutoka kwa wafuasi wake tangu alipoanza kushikilia kufanyika udaganyifu wa kura nchini Marekani. Fedha hizo zote zimeingizwa kwenye mfuko binafsi wa Trump alioupajina la Mfuko wa Kamati ya Misaada ya Pamoja.

Shirika la habari la IRIB limevinukuu vyombo vya habari vya Magharibi ikiwemo televisheni ya CNN na gazeti la New York Times vikisema kwamba wafuasi wa Trump wameshamkusanyia Trump dola milioni 170 tangu alipoanza kushikilia kuweko udanganyifu katika uchaguzi wa Marekani.

Huku hayo yakiripotiwa, Bernard Sanders, seneta wa jimbo la Vermont la kaskazini mashariki mwa Marekani amesema kuwa, Donald Trump ndiye rais hatari zaidi kuwahi kuitawala Marekani.

Wanamgambo wa Donald Trump

 

Sanders ameandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba Donald Trump amedharau mateso wanayopata wananchi wa Marekani kutokana na ugonjwa hatari wa corona na amezidi kuthibitisha kwamba yeye ndiye rais hatari zaidi kuwahi kuingia katika ikulu ya nchi hiyo White House.

Habari nyingine kutoka Marekani imemnukuu Waziri wa Mahakama na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa nchi hiyo William Barr, akisema kuwa, hakuna ushahidi wowote wa kuthibitisha kuweko udanganyifu mkubwa wa kura za uchaguzi wa Novemba 3, 2020 nchini humo kinyume na anavyodai Donald Trump.

Shirika la habari la Associated Press limemnukuu Barr akisema hayo jana licha ya kwamba Donald Trump anaendelea kushikiliza msimammo wake wa kuweko uchakachuaji mkubwa wa kura katika uchaguzi wa hivi karibuni nchini Marekani.

Tags