Dec 03, 2020 04:38 UTC
  • Iran yataka mshikamano wa dunia katika kukabiliana na hatua za kimabavu

Balozi na mwakilishi wa kudumu wa Iran katika taasisi za kimataifa mjini Vienna, Austria ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuwa na mshikamano katika kukabiliana na hatua za kimabavu za upande mmoja.

Kazem Gharibabadi, Balozi na Mwakilishi wa Kudumu wa Iran katika taasisi za kimataifa mjini Vienna ameyasema hayo katika Semina ya Wanadiplomasia kuhusu "Hatua za Kimabavu za Upande Mmoja Katika Kipindi cha Corona', ambayo iliandaliwa na wawakilishi wa Iran, Cuba na Venezuela mjini Vienna na kuhudhuriwa na wawakilishi wa nchi zaidi ya 38.

Katika hotuba yake, Gharibabadi  amesema katika miaka ya hivi karibuni, kumeshuhudiwa baadhi ya nchi, hasa Marekani, zikifikia malengo yao ya sera za kigeni kwa kuchukua hatua za upande mmoja  na za kimabavu dhidi ya nchi zingine.

Gharibanadi amesema hatua haramu za kimabavu za Marekani zimechangia katika kudhoofisha jitihada za kukabiliana na maambukizi ya corona na kuongeza kuwa, sera hizo za Marekani za utumiaji mabavu zimeathiri vibaya sana afya na maisha ya watu wa mataifa mengi duniani.

Tags