Dec 03, 2020 04:42 UTC
  • Balozi wa Russia UN: Tuzuie kukaririwa vita vikuu vya dunia

Mwakilishi wa Kudumu wa Russia katika Umoja wa Mataifa Vasily Alekseevich Nebenzya ametoa wito kwa jumuiya za kimataifa na nchi za dunia kuchukua hatua za kuzuia kukaririwa tena vita vikuu vya dunia ambavyo viliandamana na mauaji ya mamilioni ya watu.

Balozi Nebenzya ameyasema hayo alipohutubu katika kikao cha Baraza  Kuu la Umoja wa Mataifa ambacho kiliitishwa kuwakumbuka waliofariki dunia katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia ambapo ametoa wito wa kuzuiwa kukaririwa tena vita kama hivyo.

Ameendelea kusema: "Sisi tunapaswa kuzuia kukaririwa mauaji ya kivita duniani. Tunapaswa kufanya hivyo kwa ajili ya kuwaenzi wale waliouawa katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia."

Mwanadiplomasia huyo wa Russia amesema jukumu la kuzuia kuenea fikra za  kinazi liko mikononi mwa serikali. Aidha amesema jamii ya kimataifa inapaswa kuwa macho na kundamiza fikra za kinazi.

Vita Vikuu vya Pili vya Dunia

Watu milioni 70-85 wanakadiriwa kupoteza maisha katika Vita Vikuu vya Dunia. Vifo vilivyotokana moja kwa moja na vita vinakadiriwa kuwa milioni 50-56 na vifo vilivyotokana na matatizo ya njaa na magonjwa ambayo yalisababishwa na vita vinakadiriwa kuwa milioni 50–56. Vita hivyo vilianza Septemba 1, 1939 na kumalizika Septemba 2, 1945

Tags