Dec 04, 2020 04:36 UTC
  • Mahakama Marekani: Uchunguzi ufanyike kuhusu hali isiyo ya kibinadamu ya watoto wahajiri nchini humo

Mahakama moja nchini Marekani imetaka kufanyika uchunguzi kuhusu watoto waliohajiri nchini humo na kisha kutenganishwa na familia zao.

Mahakama hiyo imeiagiza kamati teule ya uchunguzi iendelee kufanya uchunguzi ili kuwapata wazazi wa watoto 628 ambao walitengenishwa katika mpaka wa Mexico na nchi hiyo kwa amri ya Rais Donald Trump. 

Familia za wahajiri kutoka Mexico katika kivuko cha mpaka na Marekani 

Mahakama hiyo ya nchini Marekani aidha imeitaka serikali ya Federali kuandaa maelezo ya kina pia kwa ajili ya kufikia natija kazi iliyopewa kamati hiyo ya uchunguzi mbali na namba za simu zilizowasilishwa kwa kamati hiyo wiki iliyopita. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, baadhi ya familia za watoto hao wanaishi Marekani na wengine nje ya nchi hiyo. 

Watoto hao walitengana na wazazi wao maeneo ya mpakani, kisha wazazi baba na mama zao walishtakiwa kwa mujibu wa kile kinachotajwa kama "siasa za kutokuwa na uvumilivu za Donald Trump katika kuamiliana na wahajiri haramu huko Marekani.  

Serikali ya Trump tarehe 25 Novemba mwaka huu hatimaye ilikabidhi kwa kamati teule ya uchunguzi namba za simu na taarifa nyingine ambazo ziliwalishwa kwa Wizara ya Sheria ya Marekani na tovuti ya hifadhi data ya ofisi inayoshughulia masuala ya wahajiri.  Lee Glerant mwanachama wa Muungano wa  Jumuiya za Kiraia za Marekani na ambaye pia ni Wakili wa Familia amesema kuwa, taarifa hizo zimepatikana baada ya kuishinikiza serikali ya Trump kwa zaidi ya mwaka mmoja. 

Siasa hizo zisizo za kibinadamu za Trump alizozitekeleza katika miaka ya karibuni dhidi ya wahajiri huko Marekani zimepingwa vikali na kukosolewa pakubwa na wanaharakati wa kiraia na makundi ya kutetea haki za wahajiri ndani ya nje ya nchi hiyo. 

Tags