Dec 04, 2020 04:39 UTC
  • Jumuiya za haki za binadamu: Biden akomeshe uungaji mkono wa fedheha wa Marekani katika vita huko Yemen

Jumuiya za kutetea haki za binadamu zaidi ya 80 zimemwandikia barua ya pamoja Rais mteule wa Marekani na kumtaka ahitimishe uungaji mkono wa fedheha wa Washington kwa muungano vamizi huko Yemen unaaongozwa na Saudi Arabia.

Katika barua yao hiyo ya pamoja kwa Biden, jumuiya hizo za haki za binadamu zaidi ya 80 za nchini Marekani zimeashiria hali ya maafa ya kibinadamu yaliyosababishwa na vita vya muungano vamizi huko Yemen unaoongozwa na Saudi Arabia na matatizo mbalimbali yanayoikumba nchi hiyo kutokana na kuenea  maambukizi ya corona nchini humo.  

Barua hiyo imebainisha kuwa Yemen ilikuwa tayari imeathiriwa na maafa ya kibinadamu hata kabla ya kuenea maambukizi ya virusi vya corona. Jumuiya hizo za Marekani zimeashiria pia mashambulizi ya mara kwa mara ya muungano vamizi wa Saudia kwa miundombinu na vituo vya huduma za afya huko Yemen. Waaandishi wa barua hiyo wamesiistiza kuwa kuondoka Marekani katika vita vya Yemen kunapasa kuwa moja ya vipaumbele vikuu vya serikali ijayo ya Joe Biden. 

Joe Biden, Rais mteule wa Marekani  

Jumuiya hizo za haki za binadamu zaidi ya 80 za nchini Marekani zimemuandikia barua hiyo Biden katika hali ambayo akiwa katika kampeni za awali za Wademocrat katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu Biden alitamka wazi kwamba: atahitimisha mauzo ya silaha ya Marekani kwa Saudi Arabia katika kupinga vita dhidi ya Yemen.