Dec 04, 2020 04:42 UTC
  • Umoja wa Mataifa watahadharisha juu ya kuongezeka umaskini duniani kutokana na corona

Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) umetahadharisha kuwa, kuenea maambukizi ya corona kutawawafanya maskini watu wengine milioni 207 duniani.

Tovuti ya habari ya al Quds al Arabi imeripoti kuwa, Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP) jana ulitangaza kupitia utafiti uliofanywa kwamba: watu wengine milioni 207 watakuwa maskini duniani iwapo janga la corona litadumu kwa muda mrefu na mgogoro wa kiuchumi uliosabbasihwa na janga hilo kuendelea. 

Utafiti huo uliofanywa kwa mujibu wa kiwango wastani cha watu walioaga dunia kutokana na ugonjwa wa Covid-19 na tabiri za ukuaji uchumi za IMF unaonyesha kuwa, kuna uwezekano watu wengine milioni 44 pia katika miaka kumi ijayo  wakajumuishwa katika jamii ya watu maskini duniani. 

Janga la corona linavyosababisha umaskini duniani 

Serikali nyingi zikiwamo za Ulaya na pia serikali ya Marekani zimechukua hatua za kutekeleza vizuizi vya karantini na vinginenvo vya kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya corona; hatua ambazo zimepelekea kufungwa shughuli nyingi za ajira na hivyo kuibua malalamiko ya wananchi. 

Tags