Dec 04, 2020 12:14 UTC
  • UN: Jangal la COVID-19 limesababisha ongezeko la watu masikini duniani kote

Ripoti mbili kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa zimeonesha namna athari za janga la COVID-19 lilivyosababisha kuporomoka kwa nguvu ya uchumi ya watu wengi duniani na hivyo kuwaingiza katika umaskini shadidi.

Utafiti mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo, UNDP umesema, “watu zaidi ya milioni 207 wanaweza kusukumwa katika umaskini uliokithiri ifikapo mwaka 2030, kwa sababu ya athari mbaya ya muda mrefu ya janga la COVID-19, na hivyo kufanya jumla ya zaidi ya watu bilioni moja kuwa masikini.”  

Kwa mujibu wa utafiti huo, hali kama hiyo "ya uharibifu mkubwa" inaweza kumaanisha kuchelewa kuishinda COVID-19, ikitarajiwa kuwa asilimia 80 ya janga la uchumi inayosababishwa na maradhi hayo itaendelea kwa zaidi ya muongo mmoja. 

Mgonjwa wa COVID-19 akipata matibabu hospitalini

Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la Biashara na Maendeleo UNCTAD limeonya kuwa janga la COVID-19 limerejesha nyuma hatua kubwa iliyokuwa imefikiwa, kwenye upunguzaji umaskini na katika sekta za lishe na elimu. Mukhisa Kituyi, Katibu Mkuu wa UNCTAD amesema janga la COVID linazisukuma nchi maskini katika  janga lao baya zaidi la kiuchumi  katika miaka 30. Amesema Pato la Taifa, GDP linatarajiwa kushuka kwa asilimia 2.6 mwaka huu.

Tokea ugonjwa wa COVID-19 uripotiwe kwa mara ya kwanza nchini China Disemba 2019 hadi sasa, ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,400,000 duniani kote.

Tags