Dec 30, 2020 06:17 UTC
  • Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani yaafiki kuziuzia silaha Misri, Kuwait na Saudia

Katika mwendelezo wa siasa za White House zinazolenga kuuza silaha zaidi; Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani imetangaza kuwa imeafiki kutekelezwa mikataba ya kuziuzia silaha Misri, Kuwait na Saudi Arabia.

Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Marekani imetangaza kuwa, mikataba hiyo ya Washington inajumuisha kuiuzia Kuwait ndege za kivita aina ya Apache zenye thamani ya dola bilioni 4, kuiuzia Saudi Arabia mabomu erevu ya ndege aina ya GBU yenye thamani ya dola milioni 290 na kuiuzia Misri mifumo dhidi ya nishati ya joto kwa ajili ya ndege zake yenye thamani ya dola milioni 104. 

Ndege za kivita za Marekani zinaouzwa katika nchi za Kiarabu 

Nchi za Kiarabu ni miongoni mwa wanunuzi wakubwa wa silaha za Marekani. Nchi za Kiarabu za pambizoni kusini mwa Ghuba ya Uajemi kama Saudi Arabia, Imarati, Bahrain na Qatar kwa mwaka hununua silaha za mabilioni ya dola kutoka Marekani. 

Saudi Arabia katika mwaka wa kwanza ya uongozi wa Rais Donald Trump huko Marekani ilitia saini na Washington mikataba ya mabilioni kadhaa ya dola kwa ajili ya kununua aina mbalimbali za silaha na zana za kijeshi. Saudi Arabia na Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati) zinanunua silaha mbalimbali kutoka Marekani na katika nchi nyingine za Magharibi kwa ajili ya kuwaulia wananchi wasio na ulinzi wa Yemen. 

Tags