Jan 15, 2021 14:29 UTC
  • Watu kadhaa waaga dunia Norway baada ya kupewa chanjo ya Marekani

Idara ya Famasia ya Norway imetangaza kuwa raia kadhaa wa nchi hiyo wamepoteza maisha baada ya kupewa chonjo ya Pfizer iliyotengenezwa nchini Marekani.

Shirika la habari la Sputnik limeripoti kuwa watu hao 13 walipoteza maisha baada ya kudungwa chanjo hiyo ya kukabiliana na virusi vya corona ya shirika la Marekani la Pfizer.

Akizungumza na kanali ya kitaifa ya NRK mkuu wa Idara ya Famasia ya Norway amesema kati ya watu hao 13 waliopoteza maisha, 9 kati yao waliaga dunia kutokana na taathira kali za pembeni na wengine kutokana na taathira hafifu.

Amesema kwamba kwa ujumla vifo 23 vimeripotiwa na idara hiyo kutokana na chanjo za corona.

Mkuu wa idara hiyo ya famasia ya Norway huku akisema kuwa vifo ambavyo vimeripotiwa kutokana na chonjo ya corona vimehusishwa na watu wenye umri mkubwa na dhaifu kimwili amehoji iwapo kuna ulazima wa kuendelea kupewa chanjo wazee na watu dhaifu kwa madai kwamba chonjo ya Pfizer ni salama na isiyo na hatari kubwa kwa watu wa tabaka hilo au la.

Chanjo ya corona ya Pfizer

Shirika la Afya la Norway limedai kwamba ni vifo 13 tu ndivyo vimetokana na chanjo ya Pfizer.

Chanjo hiyo ilianza kutolewa nchini humo siku nne kabla ya kuanza sherehe za mwaka mpya. Kufikia sasa watu zaidi ya 33,000 wameshapewa chanjo hiyo nchini humo. Kwa mujibu wa twakwimu za Shrika la Afya Duniani WHO, zaidi ya watu 57,736 wameambikizwa corona na wengine 511 kupoteza maisha yao kutokana na virusi hivyo nchini Norway.