Jan 18, 2021 04:48 UTC
  • 55 wafariki Marekani, 13 wapooza uso Israel baada ya kupigwa chanjo ya corona

Kituo cha serikali kuu ya Marekani kinachoripoti "athari mbaya za chanjo" cha VAERS kimetangaza kuwa watu 55 wameaga dunia baada ya kupigwa chanjo ya kuzuia maradhi ya Covid-19 iliyotengenezwa na mashirika ya Pfizer na moderna.

Ripoti ya kituo hicho imeeleza kuwa, hadi sasa watu 55 wamefariki dunia baada ya kudungwa chanjo ya corona iliyotengenezwa na Pfizer na moderna na mamia mengine kadhaa ya watu wamepatwa na athari zinazohatarisha maisha yao.

Mashirika hayo mawili ya utengenezaji dawa ambayo yamepewa kibali cha kutoa chanjo ya kinga ya maradhi ya Covid-19, yamekataa kutoa jibu lolote yalipotakiwa kutoa maelezo kuhusiana na hali hiyo.

Wakati huohuo wizara ya afya ya utawala wa Kizayuni wa Israel imetangaza kuwa watu 13 waliopigwa chanjo ya corona wamepooza uso.

Mmoja wa watu waliofikwa na hali hiyo amealiambia gazeti la Kiebrania la Yediot Ahronot kwamba alipooza uso kwa muda wa masaa 28.

Upigaji chanjo ya corona ukiendelea

Wiki iliyopita, wizara ya afya ya utawala wa Kizayuni  wa Israel litangaza kuwa, idadi ya wagonjwa mahututi wa corona waliolazwa kwenye hospitali za utawala huo imefikia kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa. 

Kwa mujibu wa takwimu rasmi zilizotolewa na utawala wa Tel Aviv, hadi sasa watu 535,149 wamekumbwa na virusi vya corona na 3,910 kati yao wamefariki dunia kwa maradhi ya Covid-19 yanayosababishwa na virusi hivyo.../