Jan 20, 2021 03:11 UTC
  • China: Marekani inapaswa irudi kwenye JCPOA bila masharti yoyote

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imeitaka Marekani irudi kwenye makubaliano ya nyuklia ya JCPOA bila masharti yoyote.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Hua Chunying amesema, serikali ijayo ya Marekani inapaswa irudi, tena bila kutoa masharti yoyote, kwenye makubaliano ya JCPOA ambayo serikali ya Donald Trump ilijitoa.

Hua Chunying amesisitiza pia kwamba, Marekani inapaswa iviondoe haraka sana vikwazo vyote ilivyoiwekea Iran.

Hua Chunying

Mnamo tarehe 8 Mei 2018, Donald Trump, rais wa Marekani aliyemaliza muda wake alichukua hatua ya upande mmoja na kukiuka ahadi na majukumu ya Washington katika JCPOA kwa kuitoa nchi yake kwenye makubaliano hayo ya kimataifa sambamba na kutangaza kurejesha tena vikwazo vya nyuklia dhidi ya Iran.

Hatua hiyo ya Trump ilikosolewa na kulaaniwa vikali ndani ya Marekani na katika uga wa kimataifa.../