Jan 20, 2021 12:27 UTC
  • Mwanadiplomasia wa Russia: Serikali ya Trump kwa muda wa miaka minne imeipotosha jamii ya kimataifa kwa kusema uwongo

Mwakilishi wa Russia katika Mkutano wa Upokonyaji Silaha huko Geneva amejibu tuhuma zilizotolewa na mwanadiplomasia wa Marekani dhidi ya Russia, China na Iran na kueleza kuwa serikali ya Trump kwa muda wa miaka minne imeipotosha jamii ya kimataifa kwa kusema uwongo.

Andrei Belousov Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Russia Katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa na taasisi nyingine za kimataifa huko Geneva Uswisi amejibu tuhuma za mwanadiplomasia wa Marekani katika Mkutano wa Upokonyaji Silaha huko Geneva kwa kusema: Serikali ya Donald Trump katika kipindi cha miaka minne iliyopita imesema uwongo waziwazi ili kuhalalisha hatua haribifu za Marekani katika uga wa usalama wa kimataifa. 

Rais wa Marekani anayeoondoka madarakani, Donald Trump baada ya kushindwa uchaguzi 

Katika kikao hicho naye Marshall Billingslea Mjumbe Maalumu wa Rais wa Marekani anayehusika na udhibiti wa silaha amezituhumu Russia, China na Iran kuwa zimekiuka mapatano ya kimataifa kuhusu udhibiti wa silaha na kuzuia uenezaji wa silaha za nyuklia na kudai kuwa hatari ya hatua zinazotekelezwa na nchi hizo tatu zimepelekea mfumo mzima wa usalama wa kimataifa kukumbwa nan mgogoro mkubwa. 

Andrei Belousov amejibu pia madai haya hayo ya Mjumbe Maalumu wa Rais wa Marekani na kusisitiza kuwa: Matamshi ya jazba kama haya kutoka kwa mwakilishi wa serikali ya Trump yameshawahi kusikika huko nyuma kwa mara kadhaa katika nyuga na duru mbalimbali.  

 Serikali ya Marekani mwaka 2019 ilitangaza kujitoa nchi hiyo katika Mkataba wa Zana za Nyuklia za Masafa ya Kati (INF).