Jan 24, 2021 08:13 UTC
  • Shambulio la kigaidi katika Shirika la Mafuta la Venezuela

Rais wa Venezuela ametangaza kuwa, shambulio la kigaidi limejiri katika bomba la mafuta la shirika la mafuta na gesi la serikali la Petroleus de Venezuela na kulaani shambulio hilo ambalo limesababisha moto mkubwa.

Rais Nicolas Maduro ameeleza kuwa, Venezuela imekumbwa na shambulio la kigaidi katika bomba la kupitishia gesi na kusababisha moto mkubwa na kwamba hakuna mtu aliyepoteza maisha katika shambulio hilo. 

Wakati huo huo picha ya video kuhusu shambulio hilo la kigaidi lililotokea jana katika bomba la gesi la shirika la mafuta na gesi la Venezuela ambayo imeonyesha moto mkubwa uliotokea imerushwa katika mitandao mbalimbali ya kijamii. 

Rais Maduro wa Venezuela siku zote amekuwa akiitaja Marekani kuwa ndiyo inayohusika na oparesheni za uharibifu na kuratibu mashambulizi dhidi ya vituo vya mawasliano, nishati na taasisi za mafuta na gesi za Venezuela. 

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela 

Nicolas Maduro alishinda kiti cha urais katika uchaguzi wa  mwaka 2018 hata hivyo Marekani inaingilia masuala ya ndani ya Venezuela na imekataa kumtambua rasmi Maduro kama Rais wa nchi hiyo. Marekani aidha imeiwekea vikwazo nchi hiyo ya Amerika ya Latini na hivyo kuathiri sekta ya mafuta ya nchi hiyo. 

 

Tags