Jan 24, 2021 13:48 UTC
  • Seneta wa Republican mwenye ushawishi mkubwa: Marais wastaafu Wademocrat pia watakuja kusailiwa

Mmoja wa Maseneta wa chama cha Republican wenye ushawishi mkubwa nchini Marekjani ameonya kuwa, "marais waliopita Wademocrat" pia wataweza kuja kusailiwa iikiwa Baraza la Seneti litaendelea na mpango wake wa kumsaili aliyekuwa rais wa nchi hiyo Donald Trump.

Mchakato wa kumsaili Trump ulipitishwa mapema mwezi huu katika Baraza la Wawakilishi la Marekani baada ya baadhi ya wafuasi wake kuvamia jengo la Bunge Januari 6 wakati wajumbe wa Kongresi ya nchi hiyo walipokuwa wakikutana ili kuidhinisha rasmi ushindi wa Rais Joe Biden katika uchaguzi wa Novemba 3.

Huku baadhi ya maseneta wa chama cha Republican katika Seneti, inayotazamiwa kuanza kusikiliza kesi ya kumsaili Trump mnamo mwezi ujao wa Februari, wakikosoa vitendo vya rais huyo wa Marekani aliyemaliza muda wake, wengine kadhaa wanapinga uamuzi wa kuendelea na mchakato wa kumsaili Trump wakati ameshaondoka madarakni.

John Cornyn, Seneta mwenye ushawishi mkubwa wa Republican aliyehudumu kwenye baraza hilo kwa miaka 19 amehoji, kama ni wazo zuri kuwasaili na kuwashtaki marais ambao hawako tena madarakani, itakuja kuwaje kwa marais wa Democrat wakati Warepublican wakapopata viti vingi 2022? Lifikirieni hilo na tufanyeni lililo bora kwa nchi yetu."

Trump

Cornyn ameyasema hayo katika ujumbe alioandika kwenye mtandao wa twitter uliomlenga kiongozi wa walio wengi kwenye baraza hilo Chuck Schumer aliyesema, kutokana na wingi wa Wademocrat watanedelea na mchakato wa kumsaili Trump.

Donald Trump ni rais wa kwanza katika historia ya Marekani kusailiwa mara mbili na atakuwa wa mwanzo pia kushtakiwa baada ya kuondoka madarakani.

Baadhi ya wataalamu wa sheria nchini Marekani wamesema, ni kinyume na katiba kumshtaki kwa ajili ya kumsaili rais ambaye ameshaondoka madarakani, lakini wanasheria wengine wanasema, inaruhusika kufanya hivyo maadamu mchakato wa kumsaili umeanza kabla ya rais kumaliza kipinchi chake cha uongozi.../

 

Tags