Jan 25, 2021 02:30 UTC
  • Wamarekani wakatishwa tamaa na chanjo ya corona ya Pfizer

Baada ya kuvunja rekodi na kuongezeka sana idadi ya maambukizi na vifo vya wagonjwa wa COVID-19 nchini Marekani licha ya chanjo iliyopigiwa propaganda kubwa ya shirika la Kimarekani la Pfizer kuanza kutumika nchini humo, idadi kubwa ya wananchi wa nchi hiyo sasa wamekatishwa tamaa na utendaji kazi wa chanjo hiyo.

Kwa mujibu wa televisheni ya NBC News ya nchini Marekani, baada ya kupita siku kadhaa tangu kuanza kutolewa chanjo ya corona na shirika la madawa la "Moderna And Pfizer" la Marekani, na baada ya nchi mbalimbali duniani kununua chanjo hiyo na kuanza kuitumia, lakini utendaji kazi wake haukuwaridhisha waliopiga chanjo hizo hasa kutokana na madhara yake ya pembeni, vifo na watu kupooza viungo na kupoteza fahamu.

Kwa mujibu wa ripoti zilizowekwa kwenye mtandao wa shirikisho la Marekani wa VAERS, hadi hivi sasa watu 55 wameshafariki dunia nchini humo baada ya kudungwa chanjo hiyo ya corona ya Kimarekani iitwayo Pfizer au Moderna na mamia ya watu wamepata madhara ambayo hivi sasa yanahatarisha maisha yao.

Chanjo ya corona ya Pfizer ni hatari sana hasa kwa wagonjwa vizee

 

Mbali na Marekani, hivi sasa nchi kadhaa zilizoanza kutumia chanjo hiyo nazo zimekumbwa na hali kama hiyo ya Marekani na baadhi ya nchi zimeamua kusimamisha matumizi ya chanjo hiyo. 

Hivi sasa Marekani inaongoza dunia kwa mbali, katika maambukizo na vifo vinavyotokana na COVID-19. Watu zaidi ya milioni 25 na 569,161 wameshakumbwa na corona, na zaidi ya wagonjwa laki 4 na 27,637 wameshafariki dunia kwa ugonjwa huo nchini Marekani pekee. 

Idadi hiyo kubwa ya wagonjwa wa COVID-19 imeripotiwa na serikali ya Marekani katika hali ambayo nchi hiyo ilicherewa sana kuchukua vipimo vya COVID-19 na sasa hivi ina upungufu mkubwa wa vifaa vya tiba na maeneo ya kulazia wagonjwa na kuzikia wanaokufa kwa ugonjwa huo kutokana na idadi kubwa ya maambukizi nchini humo.

Tags