Jan 25, 2021 03:03 UTC
  • Kremlin yakosoa uingiliaji kati wa Marekani katika maandamano huko Russia

Msemaji wa ikulu ya Russia (Kremlin) ameyataja matasmhi ya uingiliaji kati ya Marekani kuhusu maandamano yaliyo kinyum cha sheria huko Russia kuwa ni uingiliaji wa masuala ya ndani ya Moscow.

Dmitry Peskov amekitaja kitendo cha ubalozi wa Marekani cha kutoa taarifa kuhusu maandamano ya juzi huko Russia kuwa ni kuingilia masuala ya ndani ya Russia. 

Msemaji wa Rais wa Russia ameeleza kuwa, ni wazi kuwa kutolewa taarifa hiyo kuhusu maandamano huko Russia ni kuunga mkono moja kwa moja ubvunjaji wa sheria na vitendo vilivyo kinyume cha sheria. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani jana ilitoa taarifa ikiunga mkono kufanyika kinyume cha sheria maandamano huko Moscow na kudai kuwa inaunga mkono juhudi za kuishinikiza Moscow katika uwanja huo. 

Ubalozi wa Marekani huko Russia pia Ijumaa iliyopita ilibainisha katika tovuti yake mahali pakufanyikia maandamano hayo yaliyo kinyume cha sheria katiak miji 20 ya Russia na wakati huo huo ikawataka raia wa Marekani kutoshiriki katika maandamano hayo.  

Wimbi jipya la mivutano limejitokeza hivi karibuni kati ya Russia na Marekani baada ya Washington kuunga mkono maandamano huko Russia kufuatia kutiwa mbaroni Alexei Navalny mkosoaji mkuu wa serikali ya nchi hiyo. 

Alexei Navalny, mkosoaji mkuu wa serikali ya Russia 

 

Tags