Feb 10, 2021 06:44 UTC
  • Mikhail Ulyanov
    Mikhail Ulyanov

Mwakilishi wa Russia katika jumuiya za kimataifa mjini Vienna amesema kuwa, ili kuweza kuhuisha makubaliano ya nyuklia ya JCPOA kuna ulazima wa serikali ya Marekani kurejea katika hali iliyokuwepo kabla ya serikali iliyoondoka madarakani ya Donald Trump bila ya masharti yoyote na kisha pande mbili za Marekani na Iran zitekeleze majukumu yao kwa mujibu wa makubaliano hayo na kufutwa vikwazo vyote vilivyowekwa dhidi ya Iran.

Mikhail Ulyanov amewaambia waandishi habari kuwa, njia pekee ya kurejeshwa hali ya kawaida ya makubaliano ya nyuklia na Iran ni kurejea katika hali ya kabla ya serikali ya Trump tena bila ya masharti yoyote.

Ulyanov ameongeza kuwa, kama kutatolewa sharti la kujadiliwa miradi ya makombora ya Iran au siasa za Tehran katika eneo la Magharibi mwa Asia itakuwa vigumu kufikia lengo la kuhuisha utekelezaji kamili wa makubaliano ya nyuklia ya JCPOA. 

Mwakilishi huyo wa Russia amesema kuwa kuna udharura wa kuwepo mawasiliano baina ya Marekani na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ingawa naelewa vyema kwamba Wairani hawako tayari kwa suala hilo; hata hivyo ni jambo linalokubalika kuitishwa kikao kisicho rasmi cha pande kadhaa katika fremu ya makubaliano ya JCPOA.

Mikhail Ulyanov

Mikhail Ulyanov mesema kuwa Russia inakaribisha hatua ya Marekani ya kubadilisha msimamo wake kuhusu makubaliano ya nyuklia ya JCPOA na iko tayari kutoa ushirikiano katika uwanja huo. 

Baada ya Marekani kujiondoa kwa upande mmoja katika mapatano ya nyuklia ya JCPOA hapo mwaka 2018, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilianzisha tena baadhi ya shughuli zake za nyuklia ikiwa ni pamoja na kuanza tena kurutubisha urani kwa asilimia 20. Iran ilichukua hatua hiyo kwa mujibu wa vipengee vya makubaliano hayo yenyewe. 

Tags