Feb 12, 2021 02:41 UTC
  • Zakharova: Moscow itachapisha nyaraka za kuhusika nchi za Magharibi katika machafuko ya Russia

Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia amesema kuwa, nchi hiyo ina azma ya kuzitumia jumuiya za kimataifa nyaraka na ushahidi wa kuhusika nchi za Magharibi katika machafuko na maandamano haramu katika miji mbalimbali ya nchi.

Maria Zakharova ambaye alikuwa akihutubia kikao cha kamati za wataalamu wa Bunge la Russia kuhusu uingiliaji kati wa nchi za kigeni katika masuala ya ndani ya nchi hiyo amesema kwamba, Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje imetarjumu za kufasiri nyaraka hizo kwa lugha zote za kigeni na itazituma katika jumuiya za kimataifa na balozi za Russia katika nchi mbalimbali ili walimwengu wajue uhakika.

Zakharova ameongeza kuwa, hatua hiyo itasaidia kuthibitisha jinsi nchi hizo zilivyoingilia masuala ya ndani ya Russia kwa kuonyesha ushahidi katika mazungumzo na washirika wa Kimagharibi. 

 Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni ya Russia amesema kuwa, suala hilo lingali linachunguzwa katika ngazi mbalimbali na kwamba hatua hiyo itabatilisha habari bandia zinazosambazwa na baadhi ya nchi za Maghariibi kuhusu kadhia hiyo na kuweka wazi ukweli kuhusu kufukuzwa wanadiplomasia wa Ulaya nchini Russia.

Maria Zakharova

Jumatatu iliyopita Ujerumani, Poland na Sweden ziliwataja wanadiplomasia watatu wa Russia waliokuwa wakifanya kazi katika nchi hizo kuwa hawatakikani na kuitaja hatua hiyo kuwa imechukuliwa kujubu hatua ya Russia ya kuwafukuza wanadiplomasia wao.

Russia iliwafukuza wanadiplomasia hao kwa kosa la kushiriki katika maandamo haramu nchini humo.

Moscow imeitaja hatua hiyo kuwa haina msingi, si ya kirafiki na haiwezi kuhalalishwa. 

Tags