Feb 15, 2021 10:55 UTC
  • Ripoti: Trump alikuwa na mpango wa kufanya mauaji ya kigaidi dhidi ya Bashar Assad

Naibu mshauri wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Marekani amefichua kuwa, rais wa zamani wa nchi hiyo, Donald Trump alikuwa na mpango wa kufanya mauaji ya kigaidi dhidi ya Rais Bashar Assad wa Syria.

Gazeti la Independent limeandika kuwa, K. T. McFarland amefichua kwamba: Baada ya kuona picha za shambulio la gesi ya sarin dhidi ya raia wa Syria, Donald Trump aliituhumu Damascus kuwa ndiyo iliyohusika na shambulizi hilo bila ya kuwa na ushahidi wowote, na kwa kutumia kisingizio hicho aliazimia kumuua kigaidi Rais Bashar Assad.  

McFarland ameongeza kuwa: Trump alinikodolea macho huku akibinya mikono yake, na wakati huo nilielewa kwamba, anataka kumuadhibu Bashar Assad. 

Donald Trump

Trump alitoa tuhuma hizo dhidi ya Syria ilhali matokeo ya uchunguzi mpya wa kituo cha utafiti cha RAND yameonyesha kuwa, awanajeshi wa Marekani walioko Iraq na Syria wameua raia karibu elfu 13 katika nchi hiyo kutokana na uzembe na kutotumia ipasavyo zana za kijeshi. 

Tags