Feb 23, 2021 13:10 UTC
  • Rais Nicolas Maduro wa Venezuela
    Rais Nicolas Maduro wa Venezuela

Viongozi wa Caracas wamelaani "vita vya kiuchumi vya pande kadhaa" za Umoja wa Ulaya na Marekani dhidi ya Venezuela.

Rais Nicolas Maduro wa Venezuela amekosoa vikwazo 450 dhidi ya nchi hiyo vilivyowekwa na Marekani na Umoja wa Ulaya na kuvitaja kuwa kinyume cha sheria, vya kisaliti na vilivyoandaliwa ili kuzidisha mgogoro wa kibindamu huko Venezuela. 

Akihutubia Kikao cha 46 cha Baraza la Usalama la UN, Rais wa Venezuela amevitaja vikwazo hivyo vya washington na Brussels dhidi ya nchi yake kuwa ni "vita vya kiuchumi vya pande kadhaa". 

Akijibu uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kuwawekea vikwazo viongozi 19 wa serikali ya Venezuela, Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Jorge Arreaza amesema hatua hiyo ni kinyume cha sheria, isiyo na msingi na iliyogonga mwamba katika jitihada zake za kufanikisha siasa za uingiliaji kati na fitina za Umoja wa Ulaya huko Caracas. 

Waziri wa Mambo ya Nje wa Venezuela, Jorge Arreaza

Jana Jumatatu Baraza la Ulaya liliyaweka majina ya viongozi 19 watajika wa serikali ya Venezuela katika orodha yake ya watu wanaokabiliwa na vikwazo kwa kisingizo kwamba viongozi hao wamehusika katika kile kilichotajwa na Umoja wa Ulaya kuwa ni maamuzi yenye kudhoofisha demokrasia na utawala wa kisheria nchini humo au yale yaliyopelekea kukiukwa pakubwa haki za binadamu. 

Tags