Feb 26, 2021 13:14 UTC
  • Russia: Mashambulio ya Marekani Syria ni ukiukaji wa kanuni na sheria za kimataifa

Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imelaani mashambulizi ya usiku wa kuamikia leo ya Marekani huko Syria na kuyataja kuwa ni kinyume na kanuni na sheria za kimataifa.

Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) jana usiku ilitangaza kuwa jeshi la nchi hiyo limeshambulia ngome za makundi ya muqawama mashariki mwa Syria kwa amri ya Rais Joe Biden wa nchi hiyo.

Mtandao wa habari wa Sabirin wenye mfungamano na makundi ya muqawama ya  Iraq pia leo Ijumaa umetangaza kuwa, ndege za kivita za Marekani zimelishambulia jengo na eneo moja jingine katika mpaka wa Iraq na Syria baina ya al Bukamal na al Qaim na  hadi sasa taarifa zinasema kuwa mtu mmoja ameuawa na wengine kadhaa wamejeruhiwa. 

Marekani na utawala haramu wa Kizayuni zimeshambulia mara kadhaa ngome za wanamuqawama katika maeneo mbalimbali huko Syria na Iraq.  

Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel zimezidisha jitihada za kuiwekea mashinikizo harakati ya muqawama baada ya harakati hiyo kuafiki kuendeleza vita dhidi ya makundi ya kigaidi katika eneo la Magharibi mwa Asia.  

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon), John F. Kirby amedai kuwa Washington imetekeleza hujuma hiyo kama jibu kwa mashambulizi ya hivi karibuni dhidi ya askari wa Marekani na waitifaki wao nchini Iraq.

Hujuma ya anga ya Marekani huko Syria 

Wanajeshi magaidi wa Marekani wako nchini Iraq tangu mwaka 2003. Mashinikizo yameongezeka ya kutaka wanajeshi hao vamizi watimuliwe nchini humo.

Tags