Apr 14, 2021 08:15 UTC
  • CODEPINK: Hujuma dhidi ya Natanz ni shambulizi dhidi ya udiplomasia wa Marekani

Wajumbe wa kundi linalopinga vita la CODEPINK wametuma ujumbe kwa Kongresi ya Marekani wakitaka kulaaniwa hujuma ya kimtandao iliyolenga taasisi za nyukli za Iran na wameitaja hujuma hiyo kuwa ni shambulizi dhidi ya udiplomasia wa serikali ya Washington.

Ujumbe huo ambao ulimwekwa kwenye mtandao wa kundi hilo jana Jumanne unasema kuwa: Baada tu ya kuanza mazungumzo baina ya Iran na Marekani, Jumapili iliyopita wakati Waziri wa Ulinzi wa Marekani, Lloyd Austin alipokuwa akifanya mazungumzo na maafisa wa Isarel, utawala huo wa Tel Aviv ulifanya hujuma ya kimtandao dhidi ya taasisi za nyuklia nchini Iran, hujuma ambayo ingeweza kusababisha kuvuja mada ya nyuklia na hata kuharibu lengo la serikali ya Joe Biden la kuhuisha mapatano ya nyuklia na Iran.

Wajumbe wa kundi linalopinga vita la CODEPINK wamesema Iran imejibu hujuma hiyo kwa kuanza uzalishaji wa urani iliyorutubishwa kwa asilimia 60. Wamewaambia wajumbe wa Kongreesi ya Marekani kwamba: Tafadhali laanini hatua na vitendo vya uharibufu vya Israel vinavyotaka kukwamisha mazungumzo ya kuhuisha mapatano ya nyukliia ya JCPOA.

Katika upande mwingine gazeti la Jerusalem Post la Israel limeripoti kuwa, kuna uwezekano kuwa "shambulizi" la Natanz limefanyika kwa shabaha ya kuathiri mazungumzo yanayoendelea huko Vienna. 

Gazeti hilo limedai kuwa, shambulizi dhidi ya taasisi muhimu ya nyuklia ya Iran huko Natanz lilipangwa muda mrefu kabla ya mazungumzo ya sasa ya nyuklia baina ya Iran na madola makubwa huko Vienna nchini Austria. 

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imelaani harakati hiyo ovu na imesisitiza haki yake ya kulipiza kisasi dhidi ya upande wowote ulioamuru na kutekeleza kitendo hicho. 

Wakati huo huo msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran ametangaza kuwa Jamhuri ya Kiislamu imeutumia barua Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki (IAEA) ikiujulisha kuwa leo inaanza operesheni ya kuzalisha madini ya urani yaliyorutubishwa kwa asilimia 60.

Msemaji wa Shirika la Atomiki la Iran ameongeza kuwa, urani iliyorutubishwa kwa asilimiai 60 inatumika katika uzalishaji wa elementi za molybdenum zinazotumiwa katika uundaji wa aina balimbali za dawa za nyuklia za radiopharmaceutical. Amesema mashinepewa mpya za IR1 zinachukua nafasi ya mashine za zamani katika urutubishaji huo.   

Jumapili iliyopita kuuliripotiwa kulishuhudiia tukio katika sehemu moja ya mtandao wa kusambaza umeme katika kituo cha kurutubisha madini ya uranium cha Shahid Ahmadi Roshan huko Natanz lakini kwa bahati nzuri tukio hilo halikusababisha maafa ya binadamu wala kuvuja kwa mionzo ya nyuklia.