Apr 17, 2021 05:40 UTC
  • Tedros Adhanom
    Tedros Adhanom

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa, maambukizi ya virusi vya corona yanaongezeka maradufu kila wiki kote duniani.

Tedros Adhanom amesema kuwa, maambukizi mapya ya virusi vya corona yamefikia kiwango cha juu zaidi tangu mlipuko wa virusi hivyo ulipoikumba dunia. 

Mkurugenzi Mkuu wa WHO amesema kuwa, baadhi ya nchi kama Papua New Guinea ambazo awali ziliweza kuzuia maambukizi makubwa ya ugonjwa wa Covid-19 sasa zimekumbwa na wimbi na ongozeko kubwa la ugonjwa huo. 

Tedros Adhanom ameongeza kuwa, mwanzoni mwa mwaka huu Papua New Guinea ilikuwa na wagonjwa 900 tu wa virusi vya corona na vifo vya watu 9 lakini sasa ina wagonjwa elfu 9 wa Covid-19 na watu wengine 83 wameaga dunia kutokana na virusi hivyo ambao nusu yao wamefariki dunia mwezi uliopita. 

Siku chache zilizopita pia Shirika la Afya Duniani (WHO) lilitangaza kuwa mwenendo wa maambukizi ya virusi vya corona duniani unaongezeka kwa kasi.

Maria Van Kerkhove

Maria Van Kerkhove Mkuu wa Kitengo cha Afya cha Huduma za Dharura katika Shirika la Afya Duniani (WHO) amesema kuwa, kasi ya maambukizi mapya ya corona duniani imeibua wawasiwa kwa viongozi duniani. 

Bi Kerkhove ameeleza kuwa karibu kesi mpya za maambukizi ya corona milioni 4.4 zilisajiliwa wiki iliyopita na kwamba, hivi sasa dunia ipo katika nukta ya mgogoro kutokana na kuongezeka kasi ya maambukizi ya corona.   

Tags