Apr 23, 2021 02:41 UTC
  • Onyo kali la Umoja wa Mataifa kuhusu hatari ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, viiongozi wa dunia lazima wachukue hatua sasa hivi na kuiweka sayari hii kwenye njia inayojali mazingira kwa sababu tunaelekea kubaya mno kwenye kuangamia kabisa sayari ya dunia.

Antonio Guterres ameongeza kuwa "Mama asili hasubiri, kwani muongo mmoja uliopita ulikuwa wenye joto zaidi katika historia na dunia inaendelea kushuhudia kupanda kwa vina vya bahari, joto kali kupita kiasi, vimbunga vikubwa vya kitropiki na moto wa aina yake wa nyikani.

Amesisitiza kuwa "Tunahitaji sayari yenye mazingira bora lakini ulimwengu uko kwenye hatua ya hatari. Tuko kwenye ukingo wa kutumbukia shimoni. Lazima tuhakikishe hatua inayofuata iko katika mwelekeo sahihi. Viongozi kila mahali lazima wachukue hatua za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi”

Hali mbaya ya hewa, New Delhi, India

 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alisema hayo jana katika kikao kilichofanyika kwa njia ya Intaneti kuhusu mazingira na kuhudhuriwa na viongozi 40 wa nchi za dunia. Amesema gesi za Green House imesababisha hatari kubwa ardhini ambayo haijawahi kutokea katika kipindi cha miaka milioni 3 iliyopita.

Marekani ndiyo iliyokuwa mwenyeji wa mkutano huo. Rais Joe Biden wa nchi hiyo ametoa  kuwa nchi yake itapunguza uzalishaji wa gesi chafu zinazoangamiza dunia. Ikumbukwe kuwa Marekani ndiye ni moja ya wazalishaji wakuu wa gesi chafu dunia ingawa muda wote imekuwa ikikataa kuheshimu juhudi za kupoambana na uharibifu wa mazingira.

Kwa upande wake televisheni ya France 24 imesema kuwa, Marekani ni ya pili kwa kuzalisha kwa wingi mno gesi chafu zinazoangamiza dunia, baada ya China. Pamoja na hayo, rais aliyepita wa Marekani, Donald Trump, aliitoa nchi hiyo katika makubaliano ya Paris ya kupambana na hali ya hewa.