Apr 23, 2021 12:02 UTC
  • Malalamiko dhidi ya marufuku ya hijabu nchini Ufaransa yaendelea

Azimio la Baraza la Seneti la Ufaransa la kuwapiga marufuku mabinti wa Kiislamu na mama zao kuvaa vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu, hijabu katika maeneo ya uma limeendelea kulalamikiwa.

Wanawake wameeendelea kujitokeza katika mitandao ya kijamii na kulalamikia hatua hiyo wanayoitaja kuwa njama dhidi ya Uislamu na matukufu yake.

Rokhaya Diallo, mwandishi wa gazeti la Washington Post katika ukurasa wa makala za kimataifa ameandika, hatua ya Ufaransa ya kupiga marufuku mabinti wa Kiislamu na mama zao kuvaa hijabu katika maeneo ya uma ni ishara ya wazi kwamba, serikali ya Paris imejikita katika kufanya dhulma na ukandamizaji dhidi ya wanawake wa Kiislamu.

Bi Rokhaya Diallo anasema: Kufuatia marufuku hiyo ya hijabu nchini Ufaransa, wanawake Waislamu wanaoishi nchini Marekani wameanzisha kampeni maalum katika mitandao ya kijamii wakiwaunga mkono wanawake Waislamu wa nchini Ufaransa.

Maandamano dhidi ya Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa mwenye chuki na Uislamu

 

Hivi karibuni pia, watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Ufaransa na maeneo mengine ya dunia walianzisha kampeni iliyopewa jina la Hands Off My Hijab (@handsoffmyhijab) wakieleza hasira zao dhidi ya azimio la Baraza la Seneti la Ufaransa la kuzidisha vizuizi na marufuku dhidi ya vazi la staha la mwanamke wa Kiislamu, hijabu.

Hivi karibuni Baraza la Seneti la Ufaransa lilipasisha marufuku ya vazi la Hijabu kwa wasichana wa Kiislamu wenye umri wa chini ya miaka 18. Baraza hilo pia limezidisha kifungu kingine katika azimio hilo ambcho kinapiga marufuku kutekeleza ibada na desturi za kidini katika vyuo vikuu vya Ufaransa. Muswada wa zimio hilo ulipendekezwa mwaka jana na Rais Emmanuel Macron wa nchi hiyo.

Tags