Apr 25, 2021 10:47 UTC
  • Pentagon: Wanajeshi wa Marekani wanashambuliwa kwa

Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, imedai kuwa, wanajeshi wa nchi hiyo wanashambuliwa na nchi za Russia na China kwa kutumia mawimbi na nishati yanayoongozwa kutoka mbali.

Ripoti iliyotumwa wiki hii na Pentagon kwenye Kongresi ya Marekani imedai kuwa, wanajeshi wa nchi hiyo katika maeneo mbalimbali ya dunia wanasumbuliwa na mashambulizi makali ya mawimbi ya redio na nishati yanayoongozwa kutokea mbali.

Vyanzo viwili vya Wizara ya Ulinzi ya Marekani vimedai kuwa, ripoti hiyo imewasilishwa kwenye Kamati ya Vikosi vya Jeshi ya Kongresi na kwamba, wanajeshi wa nchi hiyo katika pembe mbalimbali za dunia kama Syria, Afghanistan na nchi za America ya Kusini wanakabiliana zaidi na tishio hilo kuliko maeneo mengine. Imesema mashambulizi hayo yanawalenga zaidi wanajeshi wa kikosi cha kigaidi cha Marekani katika eneo la Magharibi mwa Asia kinachojulikana kwa jina la CENTCOM.

Wanajeshi vamizi wa Marekani nchini Syria

Vyanzo hivyo vimedai kuwa, Russia na China ni miongoni mwa washukiwa wa mashambulizi hayo. 

Mwaka jana Wizara ya Ulinzi ya Marekani ilianzisha uchunguzi rasmi baada ya kutolewa madai kuwa, wanajeshi wa nchi hiyo wanashambuliwa kwa mawimbi ya redio na nishati inayoongozwa kutokea mbali. 

Inadaiwa kuwa, mashambulizi hayo yanashabihiana na maradhi ambayo hayajathibitishwa ambayo mwaka 2016 yaliripotiwa katika obalozi wa Marekani nchini Cuba. Wakati huo wafanyakazi wa Kimarekani walipatwa na maumivu sugu ya kichwa na matatizo ya kusikia.       

Tags