May 09, 2021 12:04 UTC
  • Global Times: Kuingia kwenye mapigano na Russia na China ni

Gazeti la The Global Times linalochapishwa nchini China limeandika, endapo Russia na China zitaungana pamoja katika mapigano na maadui, hakuna shaka yoyote Marekani itashindwa tu.

Gazeti hilo limeeleza kuwa, serikali mpya ya Marekani inajaribu kutumia kila njia ili kuchochea, si Wamarekani pekee, bali jamii nzima ya Magharibi dhidi ya China na kusaidia kushamirisha vituo vikuu vya makabiliano duniani.

Global Times limeendelea kubainisha kwamba, "Marekani ina matumaini kuwa itaweza kuibua upinzani mkubwa wa kupinga mwenendo wa hivi sasa duniani; na kwa kufanya hivyo, itaweza kutumia nguvu zake kuasisi na kuongoza nidhamu ya dunia iliyo chini ya udhibiti wa nchi za Magharibi bila ya kuzishirikisha China na Russia."

Hata hivyo, gazeti hilo limeongeza kuwa, Wachina wanaiasa Washington isianzishe mchezo wa kistratejia wa kuchezea moto na wanaitahadharisha kwamba, nguvu za sasa za Russia na China ni kubwa mno kuliko kambi ya zamani ya kijeshi ya Shirikisho la Kisovieti la Urusi na nchi za Ulaya Mashariki.

Global Times limeeleza pia kwamba, katika hatua ya kwanza, umoja wa kistratejia wa China na Russia, ni wa kukabiliana na ubeberu wa Marekani. Kwa hivyo nchi zingine zisijiingize kati kwa kudhani kwamba kila mara Marekani itakuwa nyuma yao.../