May 10, 2021 02:57 UTC
  • Rais Putin aapa kulinda maslahi ya Russia kwa nguvu zote

Rais Vladimir Putin wa Russia ameapa kuwa atayalinda kwa nguvu zote maslahi ya taifa hilo huku akilaani vikali kile alichokitaja kuwa ni chuki dhidi ya Russia au Russophobia”.

Putin ameyasema hayo alipohutubu jana Jumapili katika gwaride kubwa la kijeshi lililoandaliwa kwa mnasaba wa  miaka 76 ya ushindi wa Vita vya Pili vya Dunia.

Akituhubia taifa katika uwanja wa Red Square, mbele ya maelfu ya wanajeshi na askari wastaafu Putin amesema Russia daima italinda sheria za kimataifa na wakati huohuo itayalinda maslahi ya taifa kwa kuhakikisha usalama wa watu wake.

Hafla hiyo inayofahamika kama Gwaride la Siku ya Ushindi, inayofanyika kila mwaka tangu kuporomoka kwa lililokuwa Shirikisho la Sovieti 1991, imefanyika pia katika miji mingine kadhaa ya Russia.

 

Makombora ya S 400 ya Russia

 

Matamshi hayo ya Putin yanakuja huku mivutano baina ya Russia na Umoja wa Ulaya pamoja na Marekani ikiongezeka sana hivi sasa.

Ijapokuwa mivutano baina ya Umoja wa Ulaya na Russia iliongezeka mwaka 2014, hata hivyo mivutano hiyo imeongezeka vibaya mno tangu alipoingia madarakani rais mpya huko Marekani, Joe Biden.