May 10, 2021 03:25 UTC
  • Baraza la Usalama la UN kukutana ili kuzungumzia matukio ya Quds inayokaliwa kwa mabavu

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kuitisha kikao leo ili kuzungumzia matukio yanayoendelea kujiri katika mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu na eneo la Sheikh Jarrah katika mji huo.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari, Baraza la Usalama litafanya kikao leo kuchunguza hali ya Baitul Muqaddas baada ya kushadidi mivutano na mashambulio ya askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Wapalestina katika msikiti wa Al Aqsa na eneo la Sheikh Jarrah.

Mashinikizo ya kimataifa yameongezeka katika siku za hivi karibuni dhidi ya utawala wa Kizayuni kuutaka ukomeshe hujuma, ukatili na ukandamzaji dhidi ya Wapalestina.

Kuhusiana na suala hilo, nchi nyingi za eneo la Asia Magharibi zimetoa matamko ya kulalamikia na kulaani vitendo vya ukatili vinavyofanywa na utawala wa Kizayuni katika eneo la Baitul Muqaddas Mashariki, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.../

Tags