May 12, 2021 00:54 UTC
  • The Guardian: Tunajuta kuunga mkono kuundwa utawala wa kizayuni wa Israel

Gazeti la The Guardian la Uingereza limeandika makala kwa mnasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 200 tangu gazeti hilo linzishwe na limeeleza majuto yake kwa kuunga mkono suala la kuanzishwa utawala wa Kizayuni wa Israel katika ardhi ya Paletina.

Katika makala ilipopewa kichwa cha maneno: "Yale Tuliyofahamu Kimakosa: Maamuzi mabaya zaidi ya Guardian katika Kipindi cha Miaka 200 Iliyopita", gazeti hilo limechambua makosa yake na kutaja suala la kuunga mkono kuundwa utawala wa Kizayuni wa Israel huko Palestina kuwa ni miongoni mwa makosa hayo.

Katika sehemu nyingine ya makala hiyo, gazeti hilo la Uingereza limeandika kuwa: "Miaka 104 iliyopita wakati aliyekuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Uingereza, Arthur Balfor alipotoa ahadi ya kusaidia kuundwa nchi kwa ajili ya Wayahudi huko Palestina, maneno yake yalibadili dunia." 

Makala ya The Guardian imesema, mkurugenzi wa zamani wa gazeti hilo, Scott Charles alikuwa miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa Uzayuni na kwa sababu hiyo alifumbia jicho haki za Wapalestina. 

Gazeti hilo mashuhuri la Uingereza limetangaza pia kwamba: "Israel ya leo siyo nchi iliyotabiriwa na The Guardian au liliyotaka iundwe." 

Makala hii ya Guardian imetolewa huku Msikiti wa al Asa huko Quds tukufu ukiendelea kushambuliwa vikali na askari wa utawala wa Kizayuni wa Israel. 

Maiti za raia wa Palestina waliouawa katika hujuma ya Israel

Jumatatu ya jana ndege za kivita za utawala wa Kizayuni zilishambulia maeneo kadhaa mashariki ya Ukanda wa Gaza na jengo moja la ghorofa nane la makazi ya watu magharibi mwa eneo hilo, ambapo kwa mujibu wa Wizara ya Afya ya Palestina, Wapalestina 24 wameuwa shahidi na wengine 103 wamejeruhiwa katika mashambulio hayo.     

Tags