May 19, 2021 08:25 UTC

Paul Pogba nyota wa timu ya soka ya Manchester United ya Uingereza na mwenzake Ahmad Diallo walionekana jana baada ya mechi wakiwa na bendera ya Palestina na kuonyesha uungaji mkono wao kwa wananchi wa Palestina wanaokabiliwa na hujuma na mashambulio ya kinyama ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Tukio hilo lilitokea baada ya kumaliza mechi kati ya Manchester United na Fulham katika Uwanja wa Old Trafford ambapo timu mbili hizo ziligawana pointi baada ya kutoka sare ya 1-1.

Wachezaji hao ambao wote ni Waislamu wameungana na wachezaji na wapenda haki wengine kote ulimwenguni ambao wamekuwa wakionyesha kwa namna mbalimbali himaya na uungaji mkono wao kwa Wapalestina.